Mwenyekiti wa zamani UWT kortini kwa tuhuma za kughushi cheti cha ndoa - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mwenyekiti wa zamani UWT kortini kwa tuhuma za kughushi cheti cha ndoa


Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Ilala, Norah Waziri maarufu kama Nora Mzeru amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni  akikabiliwa na tuhuma za kughushi cheti cha ndoa.

Wakili wa serikali , Benson Mwaitenda amedau leo Julai 12, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Anifa Mwingira kuwa Februari 4,1995 jijini Dar, es Salaam, mshtakiwa kwa nia ya kudanganya, alighushi cheti cha ndoa chenye usajili namba 00040078 kwa nia ya kuonesha kuwa alifunga ndoa na marehemu Silvanus Mzeru Februari 4, 1995 katika kanisa la Roman Catholic la Mburahati huku akijua kuwa si kweli.

Hata hivyo, mshtakiwa  amekana shtaka hilo na kudai kuwa marehemu huyo ni mume wake.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na mshtakiwa yuko nje kwa dhamana baada ya kufanikisha kutimiza masharti yaliyowekwa na mahakama ambapo Mahakama imemtaka
mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili ambapo mmoja kati ya wadhamini hao atoke... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More