MWENYEZI MUNGU AKULAZE MAHALI PEMA PEPONI MZEE KING MAJUTO - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MWENYEZI MUNGU AKULAZE MAHALI PEMA PEPONI MZEE KING MAJUTO

Na Emmanuel J. Shilatu.
Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za Msiba wa Msanii nguli na Bingwa wa tasnia ya Sanaa za uigizaji na vichekesho, Amir Athuman almaarufu "King Majuto" kilichotokea usiku wa Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
Kifo hiki kimenikumbuka miaka ile ya zamani alipoanza kuwika na msemo wa hamsini, hamsini mia akiwa na muigizaji mwenzake mkongwe Marehemu Mzee Small.
Kwa wasiomjua vyema King Majuto alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini mkoani Tanga. Alianza kuigiza mwaka 1958 akiwa na umri wa miaka 9 akiigiza katika majukwaa.
Mzee Majuto maarufu kama King Majuto ni mtunzi, muigizaji, mwandishi wa mswada. Pia Mzee Majuto ni muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC).
Kwa sasa King Majuto ni mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki.
King Majuto... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More