MWILI WA ALIYEKUWA DIWANI WA KATA YA MAGOMENI MHE DKT.JULIAN BUJUGO AAGWA LEO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MWILI WA ALIYEKUWA DIWANI WA KATA YA MAGOMENI MHE DKT.JULIAN BUJUGO AAGWA LEO

Akiongoza shughuli hiyo ya kuaga mwili wa aliekua Diwani Kata ya Magomeni Manispaa ya Kinondoni Dkt.Julian Bujugo  iliyohudhuriwa pia na viongozi wa vyama na Serkali,  Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni  Mh.Benjamini Sitta amesema,  Kinondoni imepoteza mpiganaji, mpenda haki, mtetezi wa wanyonge,  na mzalendo. "Bujugo alikuwa mzalendo, alikuwa ni mtu aliyependa kuona mambo yanakwenda, wanyonge wanapata haki, hata siku ambayo usiku wake mauti inamkuta, Mh Bujugo alikuja ofisini kwangu mchana kwa swala la walemavu wa magomeni kuhusiana na ada ya usajili wa kikundi wanayotozwa", alisema  Meya Sitta.
Shughuli hii ya kuuaga mwili wa marehemu Julian Rushaigo Bujugo imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg Aron Kagurumjuli, wakuu wa idara na vitengo, wananchi wa kata ya Magomeni, pamoja na viongozi wa vyama na serikali, akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bi.Kate Kamba, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Ndg. Harold Maruma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam M... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More