Mwili wa Mchezaji wa Mpira SALA Aliyepata Ajali ya Ndege Wapatikana - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mwili wa Mchezaji wa Mpira SALA Aliyepata Ajali ya Ndege WapatikanaMashabiki na wachezaji wa Soka duniani wanaomboleza na kutoa heshima zao kwa aliyekuwa mchezaji mpya wa Cardiff City, Emiliano Sala baada ya mwili wake kupatikana ndani ya masalia ya ndege iliyopotea mwezi uliopita.

Januari 21, Sala alikuwa akisafiri kwa ndege binafsi akitokea katika klabu yake ya zamani Nantes ya Magharibi mwa Ufaransa akielekea Cardiff kuanza rasmi kazi ya kukitumikia kikosi hicho katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Mabaki ya ndege pamoja na mwili wa Sala yalipatikana kufuatia utafutaji wa kina uliohusisha watalaam uliofadhiliwa na watu binafsi baada ya Mamlaka za Serikali kueleza kuhitimisha zoezi la awali la utafutaji.

“Mwili umewasilishwa leo katika Bandari ya Portland na umethibitishwa na Mamlaka ya Dorset kuwa ni wa mchezaji huyo wa kulipwa, Emiliano Sala ambaye ni raia wa Argentina,” imeeleza taarifa ya Polisi.

“Familia ya Sala na rubani David Ibbotson zimejulishwa kuhusu hatua iliyofikiwa na wamekuwa wakihudumiwa kwa ukaribu na kitengo maalum cha maafa na masuala ... Continue reading ->

Source: Mwanaharakati MzalendoRead More