Mwili wa Pancho Waagwa Lugalo Tayari Kwenda Gairo. - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mwili wa Pancho Waagwa Lugalo Tayari Kwenda Gairo.

MASTAA, wadau wa sanaa ya muziki na waombolezaji mbalimbali wamejitokeza leo Ijumaa, Oktoba 12, 2018, kuaga mwili wa aliyekuwa Producer wa Studio za H-Bits, Pancho Latino, katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar.


Pancho maarufu kama Mafia, alifariki dunia juzi jioni kwenye ajali ya kuzama na maji wakati akiogelea kwenye Kisiwa cha Mbudya jijini Dar es Salaam.


Mwili wa marehemu umeagwa leo Dar na katika ibada maalum ya kuaga na utasafirishwa kwenda nyumbani kwao Gairo, mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi, kama ilivyotangazwanhapo awali na baba wa marehemu .


Pancho anasemwa kama moja ya watayarishaji bora wa muziki nchini Tanzania , hivyo tasnia imepoteza mtu bora na muhimu sana.


The post Mwili wa Pancho Waagwa Lugalo Tayari Kwenda Gairo. appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More