MWIMBAJI EMMANUEL MBASHA ATOA POVU MAOMBEZI YA MWIMBAJI ROSE MUHANDO - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MWIMBAJI EMMANUEL MBASHA ATOA POVU MAOMBEZI YA MWIMBAJI ROSE MUHANDO

Nikiwa kama baba wa kiroho na mlezi mkuu wa waimbaji wote wa nyimbo za injili Tanzania, napenda kuweka wazi kuwa nimehuzunishwa sana na hii video ya maombezi ya muimbaji mwenzetu Rose Muhando.
Kwa unyenyekevu kabisa naweza kusema kuwa, maombi ni muhimu sana kwa watu wote, ila namna ya kuombea ikiwa mbaya inaweza kuharibu umuhimu wote wa maombi na kusababisha maombi yadharaurike au yamdharaulishe aliyeombewa.
Katika nia yangu ya ndani nimefurahishwa sana na kitendo cha Rose kuombewa, ila kero yangu kubwa imekuwa kwenye njia iliyotumika kumuombea.
Rose Muhando ni star, na katika medani za mziki wa injili ni mtu anaetazamwa na watu wengi sana kama rol model wao, hivyo nadhani ilikuwa ni bora zaidi kuwa waangalifu katika kumuombea ili kulinda brand yake.
Biblia inasema, mwenye heshima apewe heshima, hivyo kwangu mimi sidhani kama mchungaji aliyemuombea Rose amempatia heshima anayostahili, maana binafsi sikuona haja ya kuwasha camera na kuanza kumuombea hadharani vile.
Hali hii inaweza kumtangaz... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More