Mzambia wa Lwandamina ampagawisha Manara - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mzambia wa Lwandamina ampagawisha Manara

Ofisa habari wa Simba Maji Manara amepagawishwa na uwezo wa kiungo wao mpya Cletus Chota Chama waliyemsajili Dynamos ya Lusaka Zambia kutokana na uwezo wake mkubwa uwanjani.


Manara amesema, Chama ambaye pia amewahi kuichezea Zesco United anaweza kuufananisha uwezo wake na gwiji Hamis Thobias Gagalino ambaye alitamba kwenye soka la Tanzania miaka ya nyuma.


“Tumefanya usajili tumemleta mtu anaitwa Chama, ebwana sio kama namsifu lakini kwa namna nilivyomuona, hapa ana miezi sita akizidisha sana mwaka anaondoka kwenda mbele, anajua mpira hadi anakera. Huyo mtu ni balaa labda naweza kumfananisha na Gagalino, Okwi, Bocco, Kagere watakuwa wanafunga hadi wanaona tabu”-Haji Manara.


Angalia full video kupitia Dauda TV kuona Haji Manara alivyopagawishwa na mchezaji mpya wa Simba Chama.


... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More