Mzimu wa Ole Gunnar waendelea kuitafuna PSG, baada ya Neymar sasa zamu ya Cavani kuikosa Manchester United UEFA - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mzimu wa Ole Gunnar waendelea kuitafuna PSG, baada ya Neymar sasa zamu ya Cavani kuikosa Manchester United UEFA

Edinson Cavani huenda akakosa mechi ya mkondo wa kwanza ya vilabu bingwa dhidi ya Manchester United. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anauguza jeraha katika kiuno chake baada ya kufunga mkwaju wa penalti katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Bordeaux. Mshambuliaji mwenza Neymar hatoshiriki katika mkondo wa kwanza wa mechi hiyo na ule wa pili mnamo tarehe 6 mwezi Machi.

Kwa mujibu wa BBC. Katika taarifa PSG imesema kuwa kutopatikana kwa Cavani kutategemea jeraha lake katika siku chache zijazo. Akizungumza na runinga ya Ufaransa siku ya Jumapili, mkufunzi Thomas Tuchel alisema: Hakuna habari nzuri kuhusu Edi hii leo.

Aliongezea: Anafanyiwa vipimo hii leo katika kituo cha mazoezi, klabu itatoa taarifa baadaye , lakini kwa maoni yangu habari hizo haziridhishi. Itakuwa vigumu sana kumchezesha.

Kuna matumaini ya kiwango cha chini sana. Tuna matumaini lakini vipimo vya kwanza sio vizuri.

Mshambuliaji wa Brazil Neymar alipata jeraha katika ushindi wa 2-0 dhidi ya mabingwa wa kombe... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More