Mzozo wa Iran na Marekani wajadiliwa na Umoja wa Ulaya - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mzozo wa Iran na Marekani wajadiliwa na Umoja wa Ulaya

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo amewasili Brussels kuzungumzia makubaliano kuhusu mradi wa nyuklia wa Iran wakati Uingereza inatoa onyo kali dhidi ya kulipuka mzozo” bila ya kutaka” katika Ghuba.”


EU-Iran Handel | Federica Mogherini und Javad Zarif (picture-alliance/Xinhua News Agency/Li Muzi)


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo amepangiwa kukutana , pembezoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels, na mawaziri wenzake wa  Uingereza, Ufaransa na Ujerumani-madola matatu yaliyotia saini makubaliano ya mwaka 2015 yaliyoikatisha Iran matumaini ya kutengeneza silaha za nuklea ili badala yake iondolewe vikwazo.


Iran ilitangaza wiki iliyopita inasitisha utekelezaji wa baadhi ya vifungu vya makubaliano hayo, mwaka mmoja baada ya uamuzi wa rais Donald Trump wa kujitoa pamoja na kutangaza vikwazo vikali zaidi dhidi ya jamhuri hiyo ya kiislam.


Mbali na mvutano wa kidiplomasia rais Trump ameamua pia kutuma manuari ziada za kivita katika ghuba. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza Jeremy Hunt amet... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More