NAHODHA WA SERENGETI BOYS ATIMKIA DENMARK KUKIPIGA KABUMBU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NAHODHA WA SERENGETI BOYS ATIMKIA DENMARK KUKIPIGA KABUMBU

Na Agness Francis, Blogu ya JamiiMCHEZAJI wa kikosi cha Serengeti boys  Maurice Abraham ameanza majaribio katika klabu ya Midtjylland  nchini Denmark, ambao ndio mabingwa wa ligi kuu msimu uliopita 2017-18 nchini humo.
Ambapo Klabu hiyo ya Midtjylland ni matokeo ya  vilabu viwili mahasimu (Ikast na Herning) vilivyomua kuungana mwaka 1999 na kuunda klabu moja  iliyipanda daraja kucheza ligi kuu ya Denmark Danish Superliga  Mwaka 2000.
 Klabu hiyo  katika msimu wa 2014-15 ndio ilishinda taji la Danish Superliga kwa mara ya kwanza kabla ya kushinda tena taji  hilo mara ya pili msimu huo uliopita. 
Maurice a.k.a chuji ambaye ni Nahodha wa timu ya Taifa ya vijana U-17 alipata mualiko kutoka nchini Denmark kufanya majaribio katika klabu ya Midtjylland baada kuonyesha kiwango cha juu mno katika michuano ya kuwania Afcon 2019 kanda ya Cecafa ambapo Serengeti ilimaliza ikiwa imeshikilia nafasi ya tatu. 
Kocha mkuu wa Serengeti boys Oscar Mirambo ambaye pia ni kaimu mkurugenzi wa ufundi wa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More