NAIBU KATIBU MKUU AELEKEZA MIRADI YA MAJI NJOMBE KUTUMIA PAMPU ZILIZOBUNIWA NA WAZAWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NAIBU KATIBU MKUU AELEKEZA MIRADI YA MAJI NJOMBE KUTUMIA PAMPU ZILIZOBUNIWA NA WAZAWA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo ameelekeza Wataalam wa Sekta ya Maji mkoani Njombe kuanza kutumia pampu za kusukuma maji zilizobuniwa na Mzee John Fute zenye uwezo wa kusukuma maji kwa umbali wa zaidi ya mita 200 kulingana na mahitaji ya mteja bila kutumia umeme.Mhandisi Kalobelo ametoa maelekezo hayo kwa wataalam hao akiwa mkoani Njombe kwa kuwataka wafanye uchunguzi wa kupata vyanzo vya maji vinavyoweza kutumia pampu za aina hiyo ndani ya wiki moja kuanzia Juni 17, 2019 kwa lengo la kuachana na gharama kubwa za umeme zinazochangia miradi mingi ya maji vijijini kutofanya vizuri.‘‘Pampu za aina hii zinahitajika sana kwenye Sekta ya Maji kwa sasa kwa kuwawezesha wananchi walio mbali na mifumo ya miradi mikubwa ya maji kufikiwa na huduma kwa gharama nafuu kuanzia Shilingi 300,000 kulingana na mahitaji ya mteja. Tutashirikiana na COSTECH tufanye utaratibu wa kuziboresha tuanze kuzitumia mara moja.Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Kalobelo ameambatana na timu ya ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More