Naibu Waziri Biteko atatua mgogoro uchimbaji madini Tarime - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Naibu Waziri Biteko atatua mgogoro uchimbaji madini Tarime

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati mbele) pamoja na msafara wake wakiendelea na ziara katika machimbo ya dhahabu ya Msege yaliyopo wilayani Tarime mkoani Mara.
Na Greyson Mwase, Tarime
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ametatua mgogoro kwenye machimbo ya madini ya dhahabu ya Msege yaliyopo wilayani Tarime mkoani Mara kwa kuitaka kampuni inayojishughulisha na uchimbaji wa madini hayo ya Everson Limited kuhakikisha inasaini mikataba kati yake na wachimbaji wadogo wa madini wanaoendesha shughuli za uchimbaji madini na kushirikiana kwa karibu zaidi. Naibu Waziri Biteko ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea machimbo hayo leo tarehe 19 Septemba, 2018 na kusikiliza kero za wachimbai wadogo wa madini ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mikoa ya Mara na Geita yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wachimbaji wa madini.
Katika hatua nyingine, Biteko alimtaka mmiliki wa kampuni ya Everson Limited, Mwita Wambu... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More