NAIBU WAZIRI HASUNGA AONYA UKATAJI MITI HOVYO MKOANI SONGWE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NAIBU WAZIRI HASUNGA AONYA UKATAJI MITI HOVYO MKOANI SONGWENaibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga amewaonya watu wenye tabia ya kukata miti ovyo kuwa Serikali hatosita kuwachukulia hatua za kisheria kutokana na kushamiri kwa uharibifu wa misitu mkoani Songwe.

Ametoa onyo hilo wakati alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe. Amesema kufuatia kasi ya ukataji miti ovyo unaoendelea kwa ajili ya mbao na nishati ya mkaa katika maeneo hayo kunatishia kutoweka kwa mvua wanayoitegemea kwa ajili kilimo cha mazao ya kahawa, mahindi pamoja na mazao mengine.

Amewaeleza Wananchi hao kuwa uharibifu huo ukiendelea utaawathiri wao wenyewe kwa vile mvua itakoma kunyesha katika maeneo yao. Amewataka wakikata mti wapande miti na wale wanaokata miti kwa ajili ya Nishati ya mkaa wafuate kanuni na sheria ili kuepuka kukabiliana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)

Aidha, Mhe. Hasunga Amewataka Wananchi hao kuwa hata pale inapotokea wanatak... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More