NAIBU WAZIRI MABULA AMKABIDHI BIBI MASINGE HATI ZA VIWANJA VIWILI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NAIBU WAZIRI MABULA AMKABIDHI BIBI MASINGE HATI ZA VIWANJA VIWILI

Na Munir Shemweta,  MaraNaibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula amemkabidhi Bibi Nyasasi Masige  Hati za viwanja viwili vilivyopo eneo la Bunda mkoa wa Mara na kutoa onyo kwa wataalamu wa ardhi kutotoa ushauri potofu kwa viongozi wa serikali  wakati wa utekelezaji wa majukumu ya sekta ya ardhi. 
Utoaji wa hati kwa bibi Masige unafuatia bibi huyo kuwasilisha malalamiko kwa mhe Rais John Pombe Magufuli  wakati wa ziara yake katika wilaya ya Bunda mkoa wa Mara kutaka kudhulumiwa viwanja vyake. Hati za viwanja  alivyokabidhiwa bibi Masige ni za viwanja  Na 92 na  93/ Kitalu S/ Nyasula C vilivyopo katika wilaya ya Bunda mkoa wa Mara. 
Mabula alikabidhi hati hizo pamoja na hati nyingine 92 kwa wananchi wa Bunda leo akiwa katika ziara ya siku tano katika mkoa wa Mara  kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyatoa katika ziara yake ya februari mwaka huu 2018 katika mkoa wa Mara. 
Alisema serikali inategemea wataalamu katika kuendesha shughuli zake na kitendo cha ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More