NAIBU WAZIRI MABULA AWAONYA WATENDAJI WA SEKTA YA ARDHI BIHARAMULO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NAIBU WAZIRI MABULA AWAONYA WATENDAJI WA SEKTA YA ARDHI BIHARAMULO

Na Munir Shemweta, Biharamulo Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amewataka watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera kujipanga na kufanya kazi kwa bidii ili kupunguza migogoro ya ardhi na wasipotekeleza majukumu yao vizuri atawawajibisha. 
Akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Biharamulo katika ofisi za halmashauri hiyo mkoani Kagera,  Dk. Mabula alisema pamoja na changamoto zinazoikabili sekta ya ardhi katika halmashauri hiyo lakini watumishi wa sekta hiyo wanapaswa kujipanga na kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza kupunguza migogoro ya ardhi na wakati huo kuwawezesha serikali kukusanya mapato kupitia sekta ya ardhi. 
"Kama kazi haziendi migogoro ya ardhi haiwezi kuisha na ninyi hapa mna viwanja vichache lakini mmeshindwa kuviingiza katika mfumo hivyo mkimaliza kuviingiza viwanja hivyo hapo mnaweza kurekebisha takwimu" alisema Dk Mabula. 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More