NAIBU WAZIRI MASAUNI AKABIDHI MASHINE ZA KUFYATULIA MATOFALI GEREZA LA KWAMNGUMI WILAYANI KOROGWE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NAIBU WAZIRI MASAUNI AKABIDHI MASHINE ZA KUFYATULIA MATOFALI GEREZA LA KWAMNGUMI WILAYANI KOROGWE

Serikali imeyataka Magereza yote nchini kutumia Wataalamu na fursa zilizopo katika maeneo yao kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo uchache wa nyumba za askari ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli  kutaka Jeshi la Magereza liimarishe shughuli za uzalishaji kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akikabidhi mashine za kufyatulia matofali katika Gereza la Kwamngumi Wilayani Korogwe mkoani Tanga  ikiwa ni jitihada za serikali kutatua makazi ya askari nchini
Akizungumza wakati anakabidhi mashine za kufaytulia tofali kwa Uongozi wa Jeshi la Magereza mkoani Tanga, Naibu Waziri Masauni alitoa wito kwa magereza yote nchini kutumia fursa zinazowazunguka huku akiweka wazi jeshi hilo kuwa na nguvu kazi ya kutosha na wataalamu mbalimbali.
“Maagizo ya Mheshimiwa Rais Magufuli ni kuona mnatumia nguvu kazi mliyonayo ya wafungwa kuzalisha na kuweza kusimama kwa uwezo wenu wenyewe, jambo hilo linawe... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More