Naibu Waziri Mavunde aagiza uchunguzi wa malipo ya mishahara ya wafanyakazi kiwanda cha Hong Wei - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Naibu Waziri Mavunde aagiza uchunguzi wa malipo ya mishahara ya wafanyakazi kiwanda cha Hong Wei


Charles James, Michuzi TV
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amefanya ziara ya ukaguzi katika kiwanda cha HONG WEI INTERNATIONAL kilichopo Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa na kuagiza kufanyika uchunguzi katika usahihi wa malipo ya mishahara ya Wafanyakazi iliyoandikwa kwenye mikataba na kiasi halisi kinachopokelewa ambapo imeonekana kwamba kuna uwezekano mkubwa wa Serikali ikawa inapoteza mapato ya kodi ya mshahara.
Naibu Waziri Mavunde amevitaka vyombo vya uchunguzi kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mufindi kujiridhisha na nyaraka mbalimbali za mishahara ya wafanyakazi na kuwasilisha taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ndani ya siku saba.
Wakati huo huo,Naibu Waziri Mavunde amekitaka Kiwanda hicho kuwapa Wafanyakazi wote mikataba kwa mujibu wa Sheria na.6/2004 ya Ajira na Mahusiano Kazini na pia kuagiza wafanyakazi wote warudishiwe fedha walizokatwa kinyume na sheria katika mshahara wao kwa ajili ya kununua vifaa kinga na kuwataka waajiri wasikwepe jukum... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More