NAIBU WAZIRI WA MIFUGO ABDALLAH ULEGA AFUNGUA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA KATI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO ABDALLAH ULEGA AFUNGUA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA KATI

Na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amefungua rasmi maonesho ya Nane Nane Kanda ya kati ambayo yanaenda sawa na mashindano ya Nane ya Mifugo kitaifa yanayofanyika jijini Dodoma.
Ulega amefungua mashindano ya Mifugo ambayo yalianza mwaka 2011 na huwa yanafanyika Agosti 5  ya kila mwaka mkoani Dodoma na hujumuisha ng'ombe wa maziwa na nyama walioboreshwa pamoja na Mbuzi wa asili.Akizungumza jana Ulega amesema kuwa lengo kuu la mashindano hayo ni kutambua umuhimu na mchango wa rasmilimali za mifugo ya asili katika kuendeleza sekta ya mifugo nchini.
Aidha amesema kuwa mchakato huo linalenga kutambua juhudi na maarifa wanayotumia wafugaji wa mifugo ili kufuga kwa tija na hatimaye kuvutia wafugaji wengi na kuiga na kuingia kwenye ufugaji wenye tija kwa taifa.Ulega amesisitaza kuwa sekta ya mifugo ni moja ya Sekta muhimu zinazochangia kupunguza umaskini wa wananchi na kukuza uchumi wa nchi kwani ni mhimili katika kuendeleza viwanda kama ilivyoainishw... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More