NAIBU WAZIRI WA NISHATI AKABIDHI SOLAR POWER KWA ZAHANATI TATU ZA HALMASHAURI YA CHALINZE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NAIBU WAZIRI WA NISHATI AKABIDHI SOLAR POWER KWA ZAHANATI TATU ZA HALMASHAURI YA CHALINZE

Na Victor  Masangu, ChalinzeWANAWAKE  wa kijiji cha Mduma  kata Magindu  katika halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani  kwa sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kutokuwa na nishati ya umeme hivyo inawalazimu kupatiwa matibabu  kwa kutumia mwanga wa tochi au simu  pindi wanapokwenda kujifungua  katika zahanati ya Mduma  kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa maisha yao.
Wakizungumza   kijijini hapo  kuhusiana na changamoto inayowakabili wanawake hao wamesema   kwamba kwa sasa  wanapata shida kubwa wakati wa kujifungua hasa katika nyakati za usiku kutokana na kuwa na giza hivyo kuwapa wakati mgumu  wauguzi  pindi wanapotekeleza majukumu yao.
Aidha walisema  kwamba kwa kipindi kirefu katika zahanati hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbali mbali za upatikanaji wa utoaji wa huduma kwa wagonjwa hivyo wameiomba serikali ya awamu ya tano kuingilia kati suala hilo kwa lengo la kuweza kuwafikishia nishati ya umeme ambayo itakuwa ni mkombozi katika utoaji w... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More