Naibu Waziri Waitara Afunguka tatizo la mimba za utotoni - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Naibu Waziri Waitara Afunguka tatizo la mimba za utotoni

Na Charles James, Michuzi TV
LICHA ya Serikali kuweka adhabu kali dhidi ya watu wanaowasababishia ujauzito wanafunzi na watoto waliochini ya umri wa miaka 18, lakini bado tatizo la mimba za utotoni ni kubwa huku mila na desturi zikitajwa kuchangia tatizo hilo hapa nchini Tanzania.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe Mwita Waitara, wakati wa maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani, yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Idadi ya watu Duniani, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri Waitara amesema tatizo hilo ni kubwa kwa shule za msingi na sekondari ambapo ni asilimia 29 na limekua likichangiwa kwa kiasi kikubwa na mila na desturi, uendeshaji wa kesi ya kumtia mtu hatiani aliyempa mimba wanafunzi.
“Kuna mila na desturi ambazo watoto wa kike wakifikia umri fulani wanapewa chumba hivyo huko mtaani usiku kucha huwezi jua kinachoendelea, mazingira magumu ya usomaji.
“Hata katika uendeshaji kesi hizi mpaka ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More