“Naj Hakujua Kama Nabadilisha Dini”- Barakah The Prince - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

“Naj Hakujua Kama Nabadilisha Dini”- Barakah The Prince

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince ameibuka na kudai Mpenzi wake Naj hakuwa na taarifa kuwa amebadilisha dini.


Barakah amefunguka hayo Baada ya tetesi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Barakah amebadili dini kisa mpenzi wake Naj ambaye ni  Muislamu.


Katika mahojiano yake na mtandao wa Dizzim Online, Barakah ameweka wazi kuwa alipofikia uwamuzi wa kubadilisha dini hakumshirikisha mpenzi wake Naj mpaka zoezi lile lilipokamilika:Ni kweli kabisa nimebadili dini kutoka ukristo na kuwa Muislamu na hivi sasa naitwa Abdulmalik na nilifanya kwa maamuzi yangu mwenyewe kwa sababu mimi sio wa kwanza, kuna ndugu zangu kibao kwenye familia yangu wamekwisha badilisha dini na Naj mwenyewe hakujua kama nimebadilisha dini mpaka alivyoona mtandaoni, nilimficha sikutaka ajue”.Taarifa zilisambaa Kuwa huenda Barakah aliamua kubadilisha dini ili apate kufunga ndoa na mpenzi wake huyo ambaye anaishi majuu kwa sasa.


The post “Naj Hakujua Kama Nabadilisha Dini”- Barakah The Pri... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More