NANI ANAWEZA KUDHIHIRISHA NI YANGA KULIKO TARIMBA ABBAS? - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NANI ANAWEZA KUDHIHIRISHA NI YANGA KULIKO TARIMBA ABBAS?

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
HALI si shwari Yanga, baada ya Mwenyekiti wa Kamati maalumu ya kusimamia shughuli za uendeshwaji wa klabu hiyo, Tarimba Abbas kujiuzulu juzi akidai kuwa Kaimu Mwenyekiti wa klabu, Clement Sanga ni tatizo.
Siku moja baada ya hatua hiyo, jana imetoka taarifa ambayo licha ya kuwa na saini ya mtu mmoja ambaye hata hivyo, hakubainisha jina wala wadhifa wake ikisema viongozi wa matawi ya klabu ya Yanga wanamuunga mkono Sanga na wanamuona Tarimba kama msaliti na adui wa klabu hiyo.
Juni 10 mwaka huu, katika Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam, wanachama wa Yanga waliunda kamati ya watu tisa chini ya Tarimba ambaye aliwahi kuwa Rais wa klabu hiyo, kusimamia shughuli mbalimbali za klabu hiyo baada ya kile kilichoonekana kuelemewa kwa uongozi uliopo madarakani chini ya Sanga.

Tarimba Abbas amejiuzulu Uenyekiti wa Kamati maalumu ya kusimamia shughuli za uendeshwaji wa klabu ya Yanga

Katika kamati hiyo, Tarimba alikuwa anasaidiwa na Saidi Mecky Sadiki... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More