NANYAMBA SASA KUPATIWA MENEJA WAKE WA TANESCO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NANYAMBA SASA KUPATIWA MENEJA WAKE WA TANESCO

Na Veronica Simba – MtwaraWaziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ameuagiza uongozi wa juu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuteua na kupeleka Meneja atakayesimamia Halmashauri ya Nanyamba wilayani Mtwara, ili pamoja na mambo mengine aharakishe zoezi la uunganishaji umeme kwa wananchi. Alitoa agizo hilo jana, Desemba 5 akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme pamoja na kuzungumza na wananchi.
Akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Kilimanjaro, Waziri Kalemani alisema ukosefu wa Ofisi ya TANESCO katika eneo hilo, ni mojawapo ya sababu zinazochelewesha zoezi la kuwaunganishia umeme wananchi. “Najua hapa hakuna Ofisi ya TANESCO. Mtu wa kuwahudumia anatoka Tandahimba. Hivyo naagiza, kuanzia kesho awepo Meneja hapa ambaye atasimamia Nanyamba peke yake.”
Miongoni mwa majukumu makuu ambayo Waziri alielekeza yatekelezwe na Meneja atakayeteuliwa ni pamoja na kuhakikisha ndani ya siku 20 kuanzia kutolewa kwa agizo, wananchi wote waliolipia wawe wameunganishiwa huduma... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More