Napenda Kupigwa na Mpenzi Wangu- Wema Sepetu - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Napenda Kupigwa na Mpenzi Wangu- Wema Sepetu

Muigizaji wa Bongo movie supastaa Wema Sepetu ameacha watu midomo wazi baada ya kutoa Kauli ya kwamba anapenda sana pale mwanaume ambaye yupo naye kimapenzi anampiga.


Wema amedai kuwa anapokuwa Kwenye mahusiano anakuwa anaona raha pale mwanaume wake anapompiga japo kidogo pale anapokosea.


Global Publishers wanaripoti kuwa Wema Sepetu aliyasema hayo hivi karibuni kwenye sherehe ya kuzaliwa ya meneja wake, Neema Ndepanya iliyofanyika nyumbani kwa Wema, Salasala jijini Dar ambapo aliulizwa na gazeti la Ijumaa Wikienda kuhusu aina ya mwanaume anayependa kuwa nayeNapenda mwanaume anipe kipigo kidogo siyo mwanaume mnaishi miaka yote, halafu hata kukupiga kofi kidogo hakupigi”.Wema ameshawahi kusema aliyekuwa mpenzi wake Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz aliwahi kumpa kipigo cha nguvu kiasi ya kwamba alimuachia majeraha mwilini.


 


The post Napenda Kupigwa na Mpenzi Wangu- Wema Sepetu appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More