NCHI KUSIMAMA KWA DAKIKA 90 MCHEZO WA SIMBA NA AS VITA KUANZIA SAA MOJA YA USIKU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NCHI KUSIMAMA KWA DAKIKA 90 MCHEZO WA SIMBA NA AS VITA KUANZIA SAA MOJA YA USIKU

*Uwanja wa Taifa kwa Mkapa kumenoga...Simba full tambo
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
UWANJA wa Taifa jijini Dar es Salaam kumenoga!Hakuna maneno mengine ya kuelezea zaidi ya hayo wakati Tanzania ikitarajia kusimama kwa dakika 90 kushuhudia mechi kati ya Simba FC na AS Vita ya nchini Congo.
Wakati mchezo huo ukitarajiwa kuanza saa 1:00 kamili ya usiku ya leo Machi 16,2019 idadi kubwa ya mashabiki na wapenzi wa soka hasa wa Simba wamejitokeza kwa wingi kwani licha ya mchezo huo kuanza muda huo sehemu kubwa ya uwanja  umeanza kujaa.
Shangwe na nderembo zilizoambatana na tambo kwa mashabiki wa Simba zimetawala uwanjani hapa .Mashabiki wa Simba wakijipa matumaini wa kuondoka na alama tatu muhimu za mchezo  huo.
Kwa kukumbusha wakati Simba wakijigamba kushinda mechi ya leo katika mchezo wa awali uliofanyika nchini Congo Simba walipokea kichapo cha mabao 5-0.Hata hivyo mashabiki wa Simba wanasema uzuri wa mechi hizi  kila timu inauhakika wa kushinda nyumbani.Acha tusubiri.Simba shusheni presh... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More