NCHI YA URUSI WAJIANDAA KUZIMA INTANETI ILI KUJILINDA NA MAADUI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NCHI YA URUSI WAJIANDAA KUZIMA INTANETI ILI KUJILINDA NA MAADUI

Na Ripota WetuIMEELEZWA kuwa nchi ya Urusi inajipanga kuzima mtandao wa Intaneti kwa muda, kwa lengo la kujitoa katika mawasiliano na dunia kama sehemu ya majaribio yake ya kujikinga dhidi ya mashambulio ya kimtandao. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza ni kwamba mchakato huo utafanya mawasiliano baina ya raia na mashirika ya Urusi kubaki ndani ya nchi badala ya ya kupitia njia za kawaida za kimtandao kimataifa.
Tayari rasimu ya Sheria ya kuruhusu mabadiliko ya kiufundi ili kuiwezesha nchi hiyo kuendesha mtandao wake wenyewe iliwasilishwa bungeni mwaka jana wa 2018 na kwamba jaribio hilo litafanyika kabla ya Aprili 1 mwaka huu ingawa siku rasmi ya kuzimwa mtandao haijawekwa wazi itakuwa lini. Pia inaelezwa kuwa rasimu ya sheria hiyo iliyopewa jina la Programu ya Taifa ya Uchumi wa Kidijiti, inawataka watoa huduma za intaneti nchini Urusi kuwa na uwezo wa kuendelea na huduma zao hata pale ikitokea nchi za kigeni zikiamua kuitenga Urusi.
Wakati hayo yakiende... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More