'NCHI ZA AFRIKA KUENDELEA KUKABILIWA NA UHABA WA MBEGU BORA ZENYE KUTOA MAZAO MENGI' - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

'NCHI ZA AFRIKA KUENDELEA KUKABILIWA NA UHABA WA MBEGU BORA ZENYE KUTOA MAZAO MENGI'

Seif Mangwangi,ArushaNCHI za Afrika zitaendelea kukabiliwa na uhaba wa mbegu bora za msingi zenye kutoa mazao mengi na bora kutokana na uzalishaji wa mbegu hizo kuwa mdogo kulinganisha na mahitaji halisi.
Hali hiyo itaendelea kusababisha uzalishaji wa vyakula kuwa wa chini na hivyo kushindwa kukabili tatizo la njaa linalozikumba nchi nyingi barani Afrika mara kwa mara.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Meneja Masoko wa Kampuni ya kuzalisha mbegu za msingi ya Quality Basic seed yenye makao yake mkuu nchini Kenya, Wycliffe Ingoi amesema mahitaji ya mbegu bora za msingi ni kilo 156250 kwa mwaka.
Amesema kiwango hicho ni kikubwa kutokana na ugumu wa kuzalisha mbegu hizo sanjari na uwepo wa kampuni chache zinazoweza kuzalisha mbegu hizo.
" Wakulima wamekuwa wakipata mazao machache kutokana na uhaba wa mbegu za msingi na hivyo kulazimika kutumia mbegu zisizo na ubora na ambazo hazijazalishwa kitaalam, sisi kama QBS tumekuja kujaribu kumaliza hili tatizo japo kwa kiasi fulani,"am... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More