Ndege kubwa zaidi duniani yaanza kuruka, ina injini 6 na mabawa marefu zaidi ya uwanja wa mpira (+video) - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ndege kubwa zaidi duniani yaanza kuruka, ina injini 6 na mabawa marefu zaidi ya uwanja wa mpira (+video)

Ndege kubwa zaidi duniani yenye injini 6 aina ya Boeing 747 imeruka nchini Marekani kwa mara ya kwanza kwa majaribio Jumamosi ya wikiendi iliyopita.

Ndege hiyo ilifanya safari yake ya majaribio katika jangwa la Mojave, California nchini Marekani. Imeandaliwa kwa ajili ya kwenda anga ya juu kupeleka satelaiti badala ya mfumo wa roketi unaotumika sasa.

Imetengenezwa na kampuni ya uhandisi iitwayo Composites ya Scaled. Ni ndege kubwa zaidi duniani na mabawa yake mawili ni marefu zaidi kuliko uwanja wa mpira wa miguu.

Kabla ya kuruka ndege hiyo ilikuwa imefanya vipimo tu vya chini. Ilipaa kwa kasi ya kilomita 304 kwa saa (189 mph) na kufikia urefu wa mita 5,182.

“Ni ndege ya aina yake kuruka angani,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Stratolaunch, Jean Floyd na kuongeza “Hatua hii inatimiza malengo yetu na kutua mfumo mbadala zaidi na rahisi wa urushaji ndege”.

Stratolaunch ilifadhiliwa na Paul Allen, mwanzilishi mwenza wa Microsoft kama njia ya kuingia kwenye soko kwa ... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More