NDIKILO AIAGIZA HALMASHAURI YA MKURANGA KUWA MAKINI KUINGIA MKATABA NA MAWALA WABABAISHAJI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NDIKILO AIAGIZA HALMASHAURI YA MKURANGA KUWA MAKINI KUINGIA MKATABA NA MAWALA WABABAISHAJI

MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo 

NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA 
MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo ameiagiza halmashauri ya wilaya ya Mkuranga,kuwa makini na mawakala wakusanyaji wa vyanzo vya mapato ili kuepuka kukimbia na fedha hatimae kuingia kwenye migogoro na kusababisha kukimbilia mahakamani . 
Aidha ,ameitaka halmashauri hiyo kuimarisha kitengo cha ukaguzi wa ndani ili kuongeza ufanisi. Ndikilo alitoa maelekezo hayo, katika baraza maalum la madiwani kupitia hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) 2017/2018 ,wilayani Mkuranga. 
Mkuu huyo wa mkoa alitaka wajipange kupata mawakala waaminifu wasioweza kupata fursa ya kukimbia na fedha za umma. Ndikilo aliiasa halmashauri hiyo pia ,kuendelea kuongeza mapato ya ndani na kuwa na wigo wa vyanzo vya mapato ili kuinua mapato hayo. 
Pamoja na hayo, aliielekeza menejimenti wilayani hapo kuhakikisha wanatekeleza hoja 32 ambazo hazijafungwa hadi ifikapo agost 30 mwaka huu,ili ziweze kufungwa. ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More