Ndoa ya Abduli Kiba Yadaiwa Kusambaratika. - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ndoa ya Abduli Kiba Yadaiwa Kusambaratika.

Mwaka huu umekuwa ni moja ya mwaka mwema na wenye baraka kwa familia ya msanii Alikiba baada ya watoto hao wote watatu kuamua kufunga ndoa kwa mfgululizo  mwaka huu huku akianza alikba na kufuatiwa na Abduli Kiba na kisha kumaliziwa na dada yao Zabibu Kiba.


Lakini kama ilivyo kawaida kwa wasanii na watu maarufu wanakuwa wakiandamwana maneno mengi katika mitandao ya kijamii ambapo hata kabla ya harusi hizo kufungwa kumekuwa maneno mengi kuhusu wasanii hawa.


Hivi karibuni yamezuka maneno tena kuhusu moja ya ndoa hizi , hii ni ndoa ya Abduli Kiba ambae ni mdogo wake na alikiba huku ikisemekana kuwa ndo ahiyo kwa sasa imesambaratika. hii yote ni kutoana na ukweli kuwa watu wanalalamika kwanini abdul hayupo kama alikiba kwa sababu alikba amekuwa akiambatana na mkewe sehemu nyingi, lakini abdul amekuwa hafanyi hivyo.


Kila mtu amekuwa akiongea lake kuhusu msanii huyo na ndoa yake, huku wengne wakisema kuwa abdul kiba hampendi mke wake, na hata kusema kuwa inawezekana kuwa alipata shinikizo la kuoa kutoka kwa wazazi wake na wala sio chaguo lake.


Baada ya hapo GPL waliamua kumtafuta abdul kiba ili kuthibitisha tetesi hizo na ndipo Abdul kiba aliposema kuwa hawezi kuongea lakini akatoa idhini  ya kuongea na meneja wake aliyejulikana kwa jina la rehema.


Akijibu tuhuma hizo , Rehema alisema “unajua abdul ni tofauti na ali, mara nyingi anaenda kuwa huru hivyo watu wakimuona yupo anatembea mwenyewe wanajua kuwa ameachana na mke wake.na wala mke wake hajarudi nyumbani.’


Baada ya kusema hivyo , Rehema alisema kwa kuthibitisha ukweli wa mambo basi akampa mke wa Abdul Kiba simu ili aweze kuongea na mwandishi na ndipo alipompa na kuongea na mkewe Abdul Kiba na kusema kuwa tetesi hizo hazina ukweli wowote.


The post Ndoa ya Abduli Kiba Yadaiwa Kusambaratika. appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source: Ghafla TZRead More