Ndondo Cup: Uchambuzi wa Wanyama, Ngasa, Kumwembe, Lea, na Rais Karia - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ndondo Cup: Uchambuzi wa Wanyama, Ngasa, Kumwembe, Lea, na Rais Karia

Leo ilikuwa siku ya maajabu. Uzinduzi wa Ndondo cup msimu wa mwaka 2018. Mastaa kibao walikuwemo leo ikiwa ni pamoja na Viongozi wakubwa. tulipiga nao stori moja mbili tatu, Za kuhusu Ndondo pia za kuhusu kombe la dunia ikiwa ni fursa nzuri ya kujua mitazamo yao


Karibu katika uchambuzi mseto kutoka kwa wachambuzi mashuhuri pamoja na nyota mbalimbali wa kisoka kuhusiana na mitazamo yao wakilenga zaidi mwenendo wa Ndondo Cup, pia wakitudokezea machache kuhusiana na fainali za kombe la dunia kule nchini Urusi


Nilipata bahati ya kufuatilia mtanange wa wachonga samani wa Keko Maarufu kama Keko Fenicha pamoja na Wasakatonge wa Soko kuu la Mabibo Maarufu kama Mabibo maketi.


Mchezo huo ulikwenda kwa Mabibo Maketi a.k.a wauza matunda kutoa kipigo cha tatu mzuka yaani mabao matatu kwa mawili.Mbwiga mbwiguke akamtaja Nassoro Kapama mchezaji wa zamani wa Ndanda kama mchezaji bora wa mechi baada ya kuifunga Mabibo mabao mawili katika mtanange huo.


Kapama amevalia jezi namba 11Nilipata bahati ya Kuongea na mastaa kadhaa kuhusiana na mtazamo wao kwa Ndondo Cup pamoja na Kombe la dunia.

Mtu wa kwanza alikuwa Ramadhani kabwili.


Mlinda mlango huyu anayechipukia wa klabu ya Yanga alisema kuwa amefurahia kabisa kuhudhuria mchezo wake wa kwanza wa Ndondo na amepata changamoto kubwa kwani amegundua kuna vijana wanacheza mazingira magumu lakini wanajituma kama kwamba wapo ligi kuu. Timu anayoishabikia kombe la dunia ni Ujerumani lakini ameumizwa zaidi baada ya kusikia Leroy Sane ameachwa. Ameitahadharisha Brazil kwamba imejaa wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa lakini kama wasipokuwa makini wataabikia.Geoff Lea nae alitoa mtazamo wake kuhusiana na Ndondo
Kwanza amezungumia ubora wa Kapama. Ameshangazwa kwamba inakuwaje mchezaji kama Kapama hakuwa anaonekana akifanya vyema Ndanda lakini leo katika ndondo ameonesha kile ambacho wengi walitamani kuona kwake.Kwanza Geoff anaamini kuwa kuna wachezaji ambao wanahitaji kuaminika na kuachwa huru ili wafanye kile wanachohitaji kuonesha. Hivyo huenda Kapama alibanwa zaidi kwa nafasi. Hivyo JKT Tanzania wanapaswa kumwamini na kumpa nafasi kubwa.Kuhusu kuachwa kwa Leroy Sane Geoff amesema ameshangazwa sana na Maamuzi ya Jog low

makocha wengi wakibeba kombe la dunia huwa wanajiona kama malaika. Mara nyingi wanataka kuonesha kuwa kile walichokifanya hakipaswi kupingwa. Kwa mawazo yangu mimi Sane anacheza timu yoyote duniani sio Ujerumani tu


Mchambuzi maarufu wa Supersport Edo kumwembe amesema Haoni kama Ndondo Cup kucheza kwenye kiwanja kibovu ni tatizo.

Ndondo Cup ni uhalisia. Na huu ndio uhalisia wa soka letu. Tusitegemee kucheza kwenye kapeti kisha tukaiita ndondo. Vijana wanapaswa kujituma Katika mazingira magumu ili kuweza kumudi kila hali, kile kinachopita kwenye mazingira magumu huja na matunda chanyaNilipomuuliza kuhusu kuachwa kwa baadhi ya wachezaji muhimu alisema

“Kama alivyosema Lea, Makocha wengi wakishabeba ubingwa wanatuona sisi wengine hatujui kuliko wao. Kuna wakati sawa wanafanikiwa. Kwa mfano Brazil 2002 walipomuacha Romario watu wengi walilalamika sana hata raisi aliomba sana Felipe Scolari amuite Romario lakini alitemwa.kwa bahati nzuri Brazil wakabeba ubingwa. Hivyo Sane kaachwa na bado Ujerumani inaweza kubeba hivyo kukosekana kwake kusiwe na madhara.


Anko Ngasa nae alikuwepo.

Alichonifurahisha nacho tu ameniambia Ndondo ina amsha amsha kubwa kuliko hata ligi kuu. Nilishtuka kidogoNilipomuuliza kama yupo siriazi na wazo hilo akasema ndiyo, labda tu Simba na Yanga ndiyo michezo inayoizidi Ndondo kwa kuvuta mashabiki wengi uwanjani.


Kutazama video ya Ngassa hii hapa.Victor Wanyama yeye amesema anampongeza shaffih dauda na huenda akatoa zawadi kwa mshindi wa kiatu cha ufungaji bora.


(Ila Kama hujawahi kumuona Wanyama, khaaa jamaa ni bonge la mtu. Yaani kipande cha mtu)
Kweli EPL akina Ndemla na Ajibu waache kula chipsi la sivyo wakienda ulaya wakipigwa kikumbo kimoja tu tutaongea mengine.Mwisho kabisa alikuwa Raisi wa TFF.
Mh Rais Karia ameongelea mambo mengi mno. Kwanza ameomba watanzania tusiwe wanafiki. Ameomba waandishi waandike yale yenye tija na sio kuandika kwa lengo la kuchafua. Nilipomuuliza kuhusu Kombe la dunia amesema alipokuwa kijana alikuwa anaishabikia England kwa kuwa alikuwa anaipenda zaidi ligi hiyo.


“Mimi sishabikii timu za ulaya za Taifa. Mimi nashabikia timu za Afrika tu. nina imani zitafanya vyema”


Msimu huu Mo salah amenikosha sana. Nikataka nimpe promo Salah kwa raisi wetu. Nikamuuliza Mh raisi msimu huu Salah ametoa funzo gani.

Salah msimu uliopita alikuwa benchi Chelsea. Hakuwa naa msimu mzuri. Aliporudi Liverpool hakufanya makosa. Wachezaji wengi wa Tanzania wanakata sana tamaa. Ukitaka kushinda hupaswi kuacha, ukiacha hutoshinda.Ukiacha huenda ukakosa kabisa. Haijalishi upo wapi ila pambana.


Makala hii imeandaliwa na Mimi Privaldinho unaweza pia kunifollow (Instagram). Ukitaka kupata mahojiano yote ingia Dauda Tv na usishau Kusubscribe channel yetu


Source: Shaffih DaudaRead More