NEC YAIJIBU CHADEMA KUHUSU UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA BUYUNGU - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NEC YAIJIBU CHADEMA KUHUSU UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA BUYUNGU


Hussein Makame-NEC
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia amesema Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Buyungu ataendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuwa malalamiko yaliyotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kumkataa msimamizi huyo hayakufuata taratibu za kisheria.
Akitoa ufafanuzi huo jijini Dar es Salaam leo, Dkt. Kihamia alisema kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 7 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343, malalamiko hayo hayana msingi wa kisheria kwa sababu hayakuja kama rufaa ila yametolewa kama malalamiko.
“Kwa maana hiyo napenda kuwajulisha umma kwamba malalamiko haya hayamuondolei sifa Msimamizi wa Uchaguzi kwa kumuondoa kusimamia shughuli za Uchaguzi katika Jimbo la Buyungu” alisema Dkt. Kihamia na kuongeza:
“Kwa kuwa Chadema kimelalamika kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na malalamiko hayo wameyaleta kama barua, kwa kuwa kuna Kamati ya Maadili ngazi ya Taifa, malalamiko hayo yalipaswa yaletwe ndani ya muda unaokubalika am... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More