NEC YATANGAZA KUFANYIKA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA TEMEKE NA KATA 46 ZA TANZANIA BARA. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NEC YATANGAZA KUFANYIKA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA TEMEKE NA KATA 46 ZA TANZANIA BARA.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika Jimbo la Temeke, Mkoani Dar es Salaam na kwenye Kata 46 za Tanzania Bara.
Akitangaza kufanyika kwa uchaguzi huo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage amesema kuwa uchaguzi huo utafanyika Januari 19 mwaka 2019 na fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 20 Desemba 2018.
"Uteuzi wa Wagombea utafanyika tarehe 20 Desemba, mwaka huu. Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kati ya tarehe 21 Desemba, hadi tarehe 18 Januari, mwaka 2019 na siku ya uchaguzi itakuwa ni tarehe 19 Januari mwaka 2019,” amesema Jaji Kaijage.Jaji Kaijage amebainisha kuwa Tume imetangaza uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge kwenye Jimbo la Temeke baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai juu ya uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge katika jimbo hilo.
Amesema kuwa Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More