NEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATIKA KATA 21 - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATIKA KATA 21

Na Hussein Makame, NEC.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika kata 21 za mikoa 10 ya Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 16 Septemba mwaka huu.
Akitoa taarifa ya uchaguzi huo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia, alisema fomu za uteuzi wa wagombea wa uchaguzi huo zitatolewa kati ya tarehe 17 hadi 23 Agosti mwaka huu.
Aliongeza kuwa uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 23 Agosti wakati kampeni za Uchaguzi zitafanyika kati ya tarehe 24 Agosti hadi tarehe 15 Septemba mwaka huu.
Dkt. Kihamia alisema kuwa Tume imetangaza uchaguzi huo baada ya kupokea taarifa ya uwepo nafasi wazi za udiwani katika kata hizo 21 zilizopo katika Halmashauri 15 kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa.
“Nafasi wazi za udiwani katika Kata hizo zimetokana na sababu mbalimbali zikiwepo kifo, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na kufutwa uanachama” alisema Dkt. Kihamia na kuongeza kuwa;
“Baada ya kupokea taari... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More