NEC YAWATAKA WANANCHI LIWALE KUPIGA KURA AMANI NA UTULIVU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NEC YAWATAKA WANANCHI LIWALE KUPIGA KURA AMANI NA UTULIVU

Na Mwandishi wetu
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewasihi wapiga kura wote waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na wanaoishi kwenye Jimbo la Liwale mkoani Lindi na kata nne za Tanzania Bara, kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya Jumamosi Oktoba 13 mwaka huu ili kuwachagua viongozi wanaowataka wawaongoze kwa kipindi cha takribani miaka miwili ijayo. 
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage wakati akisoma risala ya uchaguzi mdogo wa jimbo hilo unaohusisha pia kata za Kibutuka katika Halmashauri ya Liwale, kata ya Korongoni katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi na Kata za Majengo na King’ori katika Halmashauri ya Meru.
Amewataka kwenda kupiga kura bila hofu, woga, wasiwasi au ushawishi kwani chini ya Kanuni ya 3.1 (b) ya Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, Serikali imepewa wajibu wa kuhakikisha kuwa kuna hali ya usalama, amani na utulivu katika kipindi chote cha Uchaguzi.
Mbali na wito huo, Jaji... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More