NEWS ALERT:BENKI KUU YA TANZANIA YASITISHA UTEUZI WA BW. FRANK NYABUNDEGE KAMA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA TIB CORPORATE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NEWS ALERT:BENKI KUU YA TANZANIA YASITISHA UTEUZI WA BW. FRANK NYABUNDEGE KAMA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA TIB CORPORATE

Kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 33(1) na 33(2) (f) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu ya Tanzania imesitisha uteuzi wa Bw. Frank Nyabundege kama Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB Corporate kuanzia tarehe 13
Julai 2019. Benki Kuu imechukua uamuzi huu kutokana na mwenendo usioridhisha wa benki ya TIB Corporate.
Kutokana na uamuzi huo, Benki Kuu ya Tanzania kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha sheria namba 33(2)(b) cha sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, imemteua Bw. Fred Luvanda kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ambaye atasimamia shughuli zote za kiutendaji za benki ya TIB Corporate.
Hatua hizi zilizochukuliwa zina lengo la kuboresha usimamizi na utendaji wa mabenki yanayomilikiwa na Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Benki Kuu ya Tanzania inauhakikishia umma kuwa benki ya TIB Corporate itaendelea kutoa huduma na madai yote yaliyoiva yatalipwa kama kawaida. Benki ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More