NEWS ALERT: Mkuu wa Soko Kuu Arusha Mbaroni kwa tuhuma za Ubadhirifu - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NEWS ALERT: Mkuu wa Soko Kuu Arusha Mbaroni kwa tuhuma za Ubadhirifu

 Na Fatuma S. Ibrahimu – Arusha Jiji  Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt. Maulid Madeni ameamuru Mkuu wa soko kuu la Halmashauri ya Jiji la Arusha Bw. John Ruzga kuwekwa chini ya ulinzi baada ya kutuhumiwa  kupokea fedha za wafanyabiashara kwa kigezo cha kwenda kuwalipia ushuru na kutozifikisha Halmashauri kitendo ambacho ni kinyume cha utaratibu wa Serikali kwa mtumishi wa umma. 
 Naye Afisa Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Bw. Baltazar Ngowi amwataka wafanyabiashara katika soko hilo kudai risiti pindi wanapolipa ushuru wa vibanda. 

 “Kutoa pesa bila kudai risiti pia ni kosa kisheria hivyo nichukue fursa hii kuwakumbusha wafanyabiashara mdai risiti pindi mnapolipa ushuru wa vibanda vyenu na mnapaswa kupeleka fedha zenu wenyewe badala ya kutuma mtu ili kuepuka kadhia ya kutapeliwa ” alisema Bw. Ngowi.
 Dkt. Madeni yupo katika wa muendelezo wa operesheni maalum ya ukusanyaji wa mapato ikiwa na lengo la kuongeza mapato ya serikali na kudhibiti matumizi mab... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More