NEWS ALERT: MO DEWJ ATEKWA NA WATU WASIOFAHAMIKA HOTELINI DAR - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NEWS ALERT: MO DEWJ ATEKWA NA WATU WASIOFAHAMIKA HOTELINI DAR

*Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar waanza msako kuhakikisha anapatikana
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii.
JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limethibitisha tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara tajiri na maarufu nchini Mohamed Dewji 'Mo'.
Mo ametekwa leo mapema asubuhi akiwa katika Hoteli ya Collessium jijini Dar  es Salaam ambako alikwenda hotelini hapo kwa ajili ya kufanya mazoezi.
Kwa mujibu wa Jeshi hilo kwa sasa wanaendelea kushughulikia suala hilo kuhakikisha Mo anapatikana na linaamini lazima apatikane.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema jeshi lake tayari limeanza kufuatilia kutekwa kwa Mo Dewji .
Wakati huo huo Kamanda wa Polisi Kanda Mkoa wa Kinondoni Ramadhan Muliro amesema jeshi hilo linaweledi wa kutosha katika kufanya kazi na hivyo wanaamini waliohusika kufanya utekaji huo watafahamika.
"Jeshi letu naliaminia sana kwa weledi hata saa 6 mchana haifiki Mo atakuwa amepatikana, sina wasiwasi kabisa katika hilo," ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More