NEWS ALERT: MWANAHABARI MKONGWE ERNEST SUNGURA ATEULIWA KUWA KIONGOZI MKUU VYOMBO VYA HABARI VYA CCM - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NEWS ALERT: MWANAHABARI MKONGWE ERNEST SUNGURA ATEULIWA KUWA KIONGOZI MKUU VYOMBO VYA HABARI VYA CCM


*Kuongoza mageuzi makubwa ya vyombo hivyo*Ni baada ya kufanya maboresho makubwa katika tasnia ya habari nchini

Na Derek Murusuri, Dar Es Salaam

USEMI maarufu katika vitabu vifakatifu kuhusu jiwe lililokataliwa na waashi kuwa jiwe kuu la pembeni, unasadifu uteuzi wa gwiji la habari nchini, Ernest Samson Sungura, kuongoza mageuzi makubwa ya vyombo vya habari vya CCM.
Habari zilizopatikana kutoka ndani ya vyombo vya habari vya CCM zinasema kuwa uteuzi wa Comrade Sungura umetangazwa leo jijini Dar Es Salaam na Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ali, ambaye alisema uteuzi huo umeidhinishwa na Kamati Kuu ya CCM.
Comrade Sungura sasa anakuwa Kiongozi Mkuu wa vyombo vya habari vya CCM, aliyepewa jukumu kubwa la kufanya mageuzi ya kimuundo na kimfumo (restructuring) ya vyombo hivyo na kuvifanya vitoe ushindani madhubuti (competitive) katika tasnia ya habari ndani na nje ya nchi.
Kabla ya uteuzi huo, Sungura alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakfu wa vyombo vya habari Tanzania (TMF) lakini aliondolewa katika taasisi hiyo na Bodi yake (TMF) muda mfupi baada ya kutangazwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC). 
Sungura ndiye mwasisi wa Tanzania Media Foundation (TMF), taasisi iliyoleta mageuzi makubwa katika tasnia ya habari nchini na kuifanya nchi jirani ya Kenya kuja kujifunza nchini kabla ya kuanzisha taasisi kama hiyo nchini mwao.Comrade Sungura ndiye anatarajiwa kuviongoza vyombo vya habari vya CCM katika mageuzi haya makubwa. Vyombo hivyo ni pamoja na televisheni, redio, magazeti na vile vya mtandaoni ambavyo katika siku za karibuni vimetokea kuwa na wafuasi wengi duniani.Pamoja na mafanikio mengine, Sungura amekuwa na rekodi nzuri na ya kipekee katika kuleta mageuzi ya kimkakati kwa taasisi za habari nchini.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA


Source: Issa MichuziRead More