NEWS ALERT: Ving’amuzi vya AZAM , ZUKU na MULTICHOICE vyatakiwa kuendelea kutoa huduma zao bila masharti yoyote - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NEWS ALERT: Ving’amuzi vya AZAM , ZUKU na MULTICHOICE vyatakiwa kuendelea kutoa huduma zao bila masharti yoyote

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

 WAZIRI wa UJenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandisi Isaac Kamwelwe amewataka watoa huduma wa ving’amuzi vya Azam, ZUKU pamoja na Multichoice kuendelea kutoa huduma zao za maudhui katika vituo vya televisheni bure kwa channel ambazo ziko katika leseni zao bila ya kuweka masharti. 

 Kamwelwe ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam kuhusiana na kadhia iliyojitokeza kwa watoa huduma hao. Amesema kuwa sheria na kanuni za nchi lazima zifuatwe kwa watoa huduma hao kutokana na masharti ya leseni walizopewa. 

 Amesema kuwa ving’amuzi vya Azam, ZUKU pamoja na Multichoice havijazuiliwa bali vitaendelea kutumika kwa mujibu wa masharti ya leseni zao walizopewa na mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Waziri wa Kamwelwe amesema utaratibu wa huduma za utangazaji kwa mfumo wa dijitali ulifikiwa baada ya maridhiano ya muda mrefu na wadau mbalimbali kwa waraka wa mashauriano na wadau hivyo lazima utaratibu uliowekwa uzingatiw... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More