NEWZ ALERT: BOSI WA ZAMANI TRA NA WENZAKE ,MTUHUMIWA WA KUiIBIA SERIKALI MIL 7 KWA DAKIKA WAACHIWA HURU,WAKAMATWA TENA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NEWZ ALERT: BOSI WA ZAMANI TRA NA WENZAKE ,MTUHUMIWA WA KUiIBIA SERIKALI MIL 7 KWA DAKIKA WAACHIWA HURU,WAKAMATWA TENA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia kesi ya utakatishaji fedha  aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya, na wenzake wawili kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea na kesi  hiyo.
Pia Mahakama hiyo imemfutia kesi mfanyabiashara aliyewahi kutajwa na Rais John Magufuli kuiibia serikali Mil.7 kwa dakika, Mohamed Yusufal na wenzake kwa sababu DPP hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Kesi hizo zote zimefutwa mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mbando na Salim Ally, baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Hashim Ngole kueleza kuwa kesi hizo leo zilikuja kwa  kutajwa.
Wakili Ngole ameeleza kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashauri hayo kwa kutumia kifungu cha 91(1) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 marejeo ya mwaka 2002.
Kufuatia taarifa hiyo, Hakimu Mmbando ameziondoa kesi hizo mbili.Hata hivyo, baada ya kutoa uamuzi huo washtakiwa wote walikamatwa na sasa wako ndani ya ukumbi wa wazi wa mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando wakisomewa mas... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More