NEWZ ALERT:MBUNGE WA MTAMA NAPE NNAUYE ANASURIKA KIFO BAADA YA GARI ALIYOKUWA AKISAFIRIA KUPATA AJALI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NEWZ ALERT:MBUNGE WA MTAMA NAPE NNAUYE ANASURIKA KIFO BAADA YA GARI ALIYOKUWA AKISAFIRIA KUPATA AJALI

Na Ripota Wetu,Michuzi Blog
MBUNGE wa Mtama Nape Nnauye(CCM) amenusurika kifo baada ya gari aliyokuwa akisafiria kupata ajali.
 Nape amepata ajali hiyo leo asubuhi katika Kijiji cha Kibutuka akiwa njiani kuelekea Liwale kwa ajili ya kushiriki kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mkoa.
Taarifa ambazo Michuzi Blog imezipata asubuhi zinaeleza kuwa ndani ya gari hiyo Nape alikuwa ameambatana na watu wengine wanne ambao wote ni wazima na hamna aliyedhurika. 
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi amepata ajali akiwa safarini kuelekea wilayani Liwale kushiriki kikao cha kamati kuu ya siasa ya mkoa wa Lindi ikiwa ni pamoja na kuungana  na ziara ya Katibu mkuu wa CCM Taifa Bashiru Ally anayoifanya wilayani Liwale. Katika ajali hiyo hakuna kifoBaadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kibutuka wakilitazama Gari lenye namba za usajiri T 349 DEL likiwa limepinduka  ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More