Neymar na wachezaji wenzake Wabrazil wamfanyia sapraizi Fred mazoezini kwa kujiunga Man United (+video) - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Neymar na wachezaji wenzake Wabrazil wamfanyia sapraizi Fred mazoezini kwa kujiunga Man United (+video)

Kiungo wa timu ya taifa ya Brazil, Frederico Rodrigues de Paula Santos maarufu kama Fred baada ya kutangazwa rasmi kusajiliwa na klabu ya Manchester United akitokea Shakhtar Donetsk, amepokelewa kwa shangwe na wachezaji wenzake wa timu ya taifa kwenye viwanja vya mazoezi vya klabu ya Tottenham jijini London ambapo timu hiyo inafanyia mazoezi tangu wiki iliyopita.


Neymar na wachezaji wengine kama Paulinho ni moja ya wachezaji waliojitokeza mapema jana kwenye mazoezi kumpongeza Fred kwa kujiunga na Man United.


Fred amejiunga na Manchester United kwa ada ya usajili wa Euro milioni 52 na ni moja ya wachezaji wenye umri mdogo walioitwa kwenye kikosi cha Brazil kinachoenda kushiriki kwenye michuano ya kombe la dunia.

Loading...Jiunge na Bongo5.com sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

The post Neymar na wachezaji wenzake W... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More