NFRA YASISITIZA HAITONUNUA MAHINDI YASIYOKUWA NA UBORA - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NFRA YASISITIZA HAITONUNUA MAHINDI YASIYOKUWA NA UBORA

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Vumilia Zikankuba
Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma
IKIWA msimu wa kununua mazao umeanza, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Vumilia Zikankuba amewataka wakulima kuhakikisha wanazingatia ubora wa mahindi.
Aidha, amesema nchi inachakula cha kutosha na kusisitiza kuwa katika msimu wa kwanza wa ununuzi wa mahindi bei ya NFRA ni wastani wa Sh 380 hadi Sh 400 kwa kilo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Dodoma, Zikankuba alisema NFRA haitaweza kununua mahindi mabovu na kusisitiza wakulima kuwa na mahindi yenye ubora ambayo yatawasaidia kupata masoko ya nje pia.
" Haiwezekani NFRA itumia fedha za Serikali kununua mahindi yasiyokidhi viwango vya ubora na machafu kutoka kwa wakulima. Hivyo wakulima wanapaswa kuzalisha mahindi kwa kuzingatia viwango vya ubora vinavyokidhi vigezo vya soko..
Aliongeza: “Lazima chakula tunachonunua kizingatie ubora. Tunataka tubadilishe t... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More