NGASSA ANG’ARA YANGA IKIICHAPA MALINDI FC 2-0 MECHI YA KIRAFIKI KUMUAGA CANNAVARO ZANZIABR LEO - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NGASSA ANG’ARA YANGA IKIICHAPA MALINDI FC 2-0 MECHI YA KIRAFIKI KUMUAGA CANNAVARO ZANZIABR LEO

Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
YANGA SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa wa Zanzibar, Malindi FC katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar jioni ya leo.
Nyota wa mchezo wa leo alikuwa mkongwe, kiungo mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa aliyefunga bao moja na kuseti moja katika ushindi huo.
Ngassa anayecheza Yanga kwa mara ya tatu baada ya kurejea tena msimu huu, alimtilia krosi nzuri Emmanuel Martin kufunga bao la kwanza dakika ya 43 kabla ya yeye mwenyewe kufunga la pili dakika ya 60 akimalizia krosi ya Pius Buswita.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Mzambia Noel Mwandila alibadili karibu kikosi chote baada ya bao la pili, lakini matokeo yakagoma kubadilika.    
Mchezo wa leo ulikuwa maalum kumuaga aliyekuwa Nahodha wake na beki hodari, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliyestaafu Mei mwaka huu.
Nadir alitokea Zanzibar kujiunga na Yanga mwaka 2006 ambako amedumu kwa miaka 12 kabla ya kutungika daluga Mei mwaka huu.
Kikosi cha Malindi kilikuwa; Ahmed Ali, Omar Yussuf... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More