NGOMA AANZA MOTO WA MABAO AZAM FC YAICHAPA 2-0 COASTAL UNION NA KUPANDA KILELENI LIGI KUU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NGOMA AANZA MOTO WA MABAO AZAM FC YAICHAPA 2-0 COASTAL UNION NA KUPANDA KILELENI LIGI KUU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
USHINDI wa mabao 2-0 ilioupata Azam FC dhidi ya Coastal Union usiku huu, umeifanya kukamata usukani wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL).
Azam FC sasa inafikisha pointi 18 baada ya kucheza mechi nane, ikishinda tano na sare tatu, mbele ya Mtibwa Sugar yenye pointi 17 mechi tisa, Yanga SC pointi 16 mechi sita, Singida United pointi 16 mechi tisa na mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 14 za mechi saba.
Alikuwa ni mshambuliaji Donald Ngoma, aliyeifyungulia ukurasa wa mabao Azam FC akifunga dakika ya 28 akitumia pasi safi ya kiungo Mudathir Yahya.
Bao hilo linamfanya Ngoma, kufungua akaunti ya mabao Azam FC tokea asajiliwe msimu huu ikiwa ni mechi yake ya tatu kuichezea Azam FC baada ya kutoka kwenye majeraha ya muda mrefu ya goti.
Kabla ya bao hilo, dakika ya 12 Ngoma alikaribia kuipatia bao jingine Azam FC baada ya kufanya kazi nzuri ya kuwahadaa mabeki wa Coastal na kupiga shuti lililopanguliwa wa kipa Hussein Shariff ‘Casillas’ na kuwa kona ambayo haikuz... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More