NGORONGORO HEROES WAENDA UGANDA KUWANIA KOMBE LA CECAFA CHALLENGE U20 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NGORONGORO HEROES WAENDA UGANDA KUWANIA KOMBE LA CECAFA CHALLENGE U20

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes kimeondoka leo Dar es Salaam kwenda Uganda kushiriki michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge U20) inayotarajiwa kuanza Septemba 21 hadi Oktoba 5 mjini Kampala.
Kikosi hicho kilicho chini ya Kocha Mkuu Zubery Katwila kimeondoka na wachezaji 25 ambao ni makipa; Ally Salim (Simba SC), Razack Shekimweki (Mtibwa Sugar) na Abdul Suleiman aliyepandishwa kutoka timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys.
Mabeki ni; Oscar Maasai (Azam FC), Andrew Simchiba (Coastal Union), Kibwana Shomari (Mtibwa Sugar), Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Dickson Job (Mtibwa Sugar) na Gustapha Simon (Yanga SC).

Viungo ni Onesmo Mayaya (Mtibwa Sugar), Ally Msengi (KMC), Kelvin Nashon (JKT), Wilbroard Maseke (Azam FC), Gadafi Said (Azam FC) na Novatus Dissmas (Biashara United).
Washambuliaji ni Kelvin John (Huru), Frank Kahole (Mtibwa Sugar), Tepso Evanc... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More