NGOs zitakazokiuka Sheria kukiona - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NGOs zitakazokiuka Sheria kukiona

Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nchini kutoka Wizara ya Afya, Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii  Neema Mwanga ametoa onya kuwa atachukua hatua kali dhidi ya Shirika lolote Lisilo la Kiserikali litalokiuka kufanya kazi kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya NGOs ya Mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005.Akiwa katika ziara ya kutembelea mashirika Yasiyo ya Kiserikali yaliyoko katika Mkoa wa Kilimanjaro Msajili Mwanga amesema kuwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanawajibu wa kuzingatia kanuni mpya za Sheria ya NGOs zinazoelekeza Mashirika hayo kufanya kazi kwa kuzingatia Misingi ya uwazi na uwajibikaji maana miradi hiyo imeanzishwa kwa lengo la kuwanufaisha wananchi ambao ndio walengwa wakuu.Msajili Mwanga aliwaambia viongozi wa Mashirika manne aliyoyatembelea leo hii ikiwemo TAWREF, White Orange, Elimu Mwangaza na Tusonge Community Organisation kwamba Misingi ya uwazi na uwajibikaji kama inavyobainishwa katika Sheria hiyo inasisitizwa kwa lengo la kukuza ushiriki wa wa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More