NHIF KAGERA YAHAMASISHA USHIRIKA AFYA KWENYE MAONESHO YA NANE NANE. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NHIF KAGERA YAHAMASISHA USHIRIKA AFYA KWENYE MAONESHO YA NANE NANE.

Na Editha Karlo,Kagera
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Kagera umewahamasisha wakulima kupitia vyama vya ushirika na masoko kujiunga na mpango wa ushirika afya (AMCOS)katika maonesho ya nane nane Mkoani humu yalifonyika katika viwanja vya Kakyailabwa (AMCOS)Kujiunga na mpango wa ushirika afya viwanja Kyakailabwa.
Akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Maico Gaguti Meneja wa Mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo alisema kuwa ushirika afya ni mpango maalum wa Bima ya afya kwa wakulima ambapo mpango huo utawawezesha wakulima kuchangia mara moja gharama za matibabu na kuwa na uhakika wa matibabu kwa mwaka mzima pale wanapougua.
Odhiambo alisema watakaojiunga na mpango huu watapata matibabu kwenye vituo vya tiba vilivyosajiliwa na mfuko nchi nzima ikiwa ni pamoja na huduma za kibingwa na vipimo.
Katika viwanja vya kyakailabwa kwenye maonyesho ya sikukuu ya nane nane banda la NHIF lilisheheni huduma mbali mbali ikiwa ni pamoja na upimaji afya ... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More