NHIF kuanza kampeni ya uandikishaji kijiji kwa kijiji - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NHIF kuanza kampeni ya uandikishaji kijiji kwa kijiji

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akionyesha kitambulisho cha matibabu kupitia mpango wa Ushirika Afya kabla ya kukabidhi kwa wanachama waliojiunga kwenye kampeni ya uhamasishaji aliyoifanya katika Mkutano wa hadhara katika eneo la Kitangali Wilaya ya Newala.

Na Grace Michael, Tandahimba
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umesema unaanza rasmi kampeni ya uandikishaji ya kijiji kwa kijiji katika Mikoa ya Mtwara na Lindi ili kuwawezesha wananchi hao kuwa kwenye utaratibu mzuri wa kupata huduma za matibabu.
Imeelezwa kuwa, wananchi wamekuwa wakiingia katika umasikini mkubwa kwa kulazimika kuuza mali za familia kwa lengo la kupata fedha za kugharamia huduma za matibabu. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Bernard Konga wilayani Tandahimba ambaye alikuwa miongoni mwa watendaji walioambatana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katika ziara yake ya kutembelea vituo vya huduma na uhamasishaji... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More